Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Novemba , 2016 (Jumanne) amefanya ziara ya
kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam na kupiga
marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka
wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.
Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa
baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za
jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini
na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja
wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini
Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini
kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili
ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi
husika.
''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na
watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu ,
amesema Rais magufuli''
click here and skip ads to learn more http://viid.me/qwTQCW
No comments:
Post a Comment