Thursday, 8 December 2016

Rais Obama kupitisha sheria ya afya

Katika Moja ya sheria za mwisho zitakazopitishwa na bunge la Marekani kabla ya Rais Barack Obama kumaliza muda wake ni muswada wa kuendelea na utafiti kuhusu magonjwa yaliyo tishio kwa binadamu, ambapo zitapelekea kuanzishwa kwa taratibu mpya za matibabu.
Rais Obama anashauku kubwa ya kupitisha sheria hiyo.
Sheria hiyo itagharimu dola bilioni sita kwa kipindi cha mwongo mmoja kwa uboreshaji wa afya, na dola bilioni moja kwa ajili ya kukabiliana madawa ya kulevya na kuboresha huduma ya magonjwa ya akili.
Sheria hizo zimeungwa mkono katika kambi zote bungeni ingawa wakosoaji wameonya kuwa inaweza kupunguza viwango vya dawa na vibali vya matibabu na kuhatarisha usalama wa mgonjwa.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews