Msemaji wa Ikulu ya White House alitaja uchunguzi huo kama hatua muhimu sana ya kutaka kujua uhuni wa hila ambao umekuwa ukifanywa na wadukuzi tangu mwaka 2008.
Matokeo ya uchunguzi huo yanapaswa kuwa yamekamilika kabla ya Rais Obama kuondoka mamlakani mwezi ujao.
Hata hivyo haijulikani iwapo matokeo hayo yatatangazwa hadharani.
Maafisa wa usalama wanadai kuwa Serikali ya Urusi ilipanga udukuzi katika barua pepe za chama cha Democratic.
Wanasema kuwa udukuzi huo ulikuwa na hila ya kutaka kuingilia shughuli za uchaguzi nchini humo.
Mrithi wa Bw Obama, Donald Trump, amesema kuwa hadhani Urusi iliingilia uchaguzi huo.
Mshauri wa Urais wa maswala ya usalama, Lisa Monaco amesema kuwa udukuzi si jambo geni lakini shughuli zake zimeimarika mwaka huu.
No comments:
Post a Comment