Kwa mjibu wa naibu kamanda mkuu wa jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika eneo la Karai kwenye barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha.
Lori moja lilianguka na kulipuka katika eneo la barabara hiyo yenye shughuli nyingi nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu 30 papo hapo.
Watu wengine zaidi walifariki wakitibiwa mjini Naivasha.
Akihutubia waandishi wa habari hii leo, waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery amesema kuwa watu 33 waliaga dunia wakimemo polisi 11 wa kikosi cha Recce ambacho humlinda rais na watu wengine mashuhuri.
Nkaisssery pia alisema kuwa sio gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali gari aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya gesi inayoshika moto kwa haraka, iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda,.
Mtu mmoja kwa jina Moses Nandalwe aliyeshuhudia ajali hiyo, ameiambia BBC kuwa, magari kadhaa yalishika moto na kuanza kuchomeka, huku watu wengi waliofika katika eneo la ajali hiyo ili kushuhudia kilichotokea, wakikumbwa na moto huo na kisha wakachomeka.
Polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo. Kuna ripoti gari aina ya Canter iligonga tuta la barabarani na kisha kuyagonga magari yaliyokuwa yakitoka upande wa mbele kabla ya kulipuka.
Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni Basi moja la matatu lililokuwa na abiria 14, ambao wanahofiwa wote wamefariki.
Ajali hiyo mbaya imetokea nchini Kenya, wakati ambapo madaktari na wauguzi wakiendelea na mgomo wao, hatua ambayo imelemaza kabisa shughuli za matibabu katika hospitali za umma.Idadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kufikia 40.
No comments:
Post a Comment