Monday 28 November 2016

Fidel Castro afariki dunia akiwa na miaka 90

Agosti 13 mwaka huu mwanamapinduzi huyo alisherehekea siku yake kuzaliwa akitimiza miaka 90 lakini jana mauti yalimkumba ghafla nyumbani kwake.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro amefariki leo akiwa na umri wa miaka 90.
Kituo cha televisheni cha serikali nchini humo kimetangaza leo kuwa mwanamapinduzi huyo alifariki saa moja asubuhi.
Kaka yake Castro, Raul Castro ambaye ndiye Rais wa sasa wa Cuba alithibitisha kifo hicho.
Agosti 13 mwaka huu mwanamapinduzi huyo alisherehekea siku yake kuzaliwa akitimiza miaka 90 na katika hotuba yake alitabiri na kusema atakufa siku za karibuni.
Castro aliondoka madarakani miaka 8 iliyopita baada ya kuugua maradhi ya tumbo.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu kifo cha mwanamapinduzi huyo.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews