Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako
amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila
kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa
masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia
kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.
Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na
kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu
hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia
(reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na
wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo
vikuu.
Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne
watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni
wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo
vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit"
za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa
diploma, na diploma zao hazitaruhusiwa kutumika kama equivalent pass ya
kujiunga chuo kukuu hadi watakaporeseat.
Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha
sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema
Foundation course haimuongezei mtu sifa.
"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha
"points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom
course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la
mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation
course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma"
Amesisitiza Ndalichako.
Unaweza kumsikiliza zaidi hapa: https://youtu.be/b5ixYuqMrnQ
Je nini maoni yako? Unakubaliana na Ndalichako au unampinga?
No comments:
Post a Comment