Wednesday 30 November 2016

Kenya kuchelewa kufunga kambi ya Daadab

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itachelewa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kwa miezi sita zaid
Kambi ya wakimbizi ya DAADAB nchini KENYA

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa itachelewa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kwa miezi sita zaidi, ili kuendelea kuwaandaa wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo kurejea nyumbani kwa amani.


Kambi hiyo ya wakimbizi ya Dadaab, kwa miongo kadhaa imekuwa ikihifadhi wakimbizi kutoka nchini Somalia waliokimbia mapigano na katika baadhi ya maeneo mengine ya Afrika.

Kenya imesema imelazimika kutofunga kambi hiyo ya wakimbizi, kutokana na ombi lililotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi -UNHCR.

Kenya ilidhamiria kufunga kambi hiyo ya wakimbizi ifikapo mwishoni na mwezi huu, lakini sasa kambi hiyo itafungwa mwezi Mei mwakani 2017.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews