Wednesday 30 November 2016

Abiria wakwama uwanja wa ndege wa SONGWE

Abiria waliokuwa wakisubiri ndege kutoka MBEYA kwenda DAR ES SALAAM, wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani MBEYA, baada ya kukosa ndege kwa siku nne sasa.

Wakizungumza Uwanjani hapo abiria hao wameiomba Serikali kuanzisha  safari ya Ndege za Serikali zilizonunuliwa hivi karibuni, kwa lengo la kumaliza matatizo yanayowakabili wasafiri na wasafirishaji kupitia usafiri wa anga kutoka MBEYA kwenda sehemu mbalimbali duniani.

Akizungumza na Viongozi wa dini waliotembelea uwanja wa ndege na maendeleo ya ujenzi, Mkuu wa mkoa wa MBEYA, AMOS MAKALA, amewahakikishia wadau wa usafiri wa anga, kuwa serikali imetoa maamuzi ya kuondoa adha ya shida ya usafiri wa anga kutoka MBEYA kwenda kwenda maeneo mengine  duniani.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa SONGWE

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews