Mashua sawia na iliyotengenezwa katika mji mkuu wa Belfast huko
Ireland ya Titanic itawekwa katika eneo la kumbukumbu la theme park
nchini India
Ujenzi huo wa mashua hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa
katika hifadhi iliyoko mashambani , katika mkoa wa Sichuan, .
Ujenzi huo uliaza siku ya Alhamisi.
Mashua ya Titanic
iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast , iligonga mwamba wa barafu
na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 hatua iliyosababisha vifo
vya zaidi ya watu 1,500.
Mashua hiyo ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Habari kuhusu meli hiyo ni swala ambalo liliwashangaza raia wengi kutoka China
isia zaidi ziliibuka mwaka 1997, baada ya filamu iliyokuwa ikimuangazia
Kate Winslet na Leonardo DiCaprio, kuwa maarufu nchini humo
Muelekezi wa filamu, James Cameron, kutoka Canada, alikuwa na mashua
kama hiyo iliotengezwa kwa maswala ya uigizaji pekee , lakini hakuna
mashua sawia na hiyo iliowahi kutengenezwa.
Bilionea mmoja
kutoka Australia, Clive Palmer, alitangaza mipango yake ya kutengeneza
mashua kama ya Titanic mwaka 2012, lakini mradi huo bado haujakamilika.
Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic ,
itakuwa na sehemu ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya
watu maalum ambayo itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa
kivutio kikubwa katika eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa
kutoka pwani ya China.
Kampuni hiyo ilitangaza mipango wa mradi
huyo, utakaogharimu Yuan bilioni moja mwaka 2014, kulingana na shirika
la habari la AFP
Utalii wa ndani nchini China umeimarika kwa kiwango kikubwa, kupitia usaidizi wa serikali.




No comments:
Post a Comment