Monday 5 December 2016

RAIS MTEULE WA GAMBIA KUWAACHILIA WAFUNGWA WA KISIASA

RAIS  MTEULE  WA  GAMBIA  AMEKUWA  AKIONGEA  JUU  YA  ANAVYOTAZAMIA  KUBADILISHA  TAIFA  TANGU  ASHINDE  BILA  KUTARAJIA  JUMA  LILILOPITA.

ADAMA  BARROW  AMBAYE  ALIKUWA  AKIFANYA  KAZI  KAMA  MFANYA  BIASHARA  WA  KUJENGA  NYUMBA  NA  KUUZA  ALIMSHINDA  , YAHYA  JAMMEH , ALIYENYAKUA  MADARAKA  KWA  MTUTU  WA  BUNDUKI  NA  KUTAWALA  KWA  MIAKA  22.

MAKUNDI  YA  HAKI  ZA  BINADAM   YAMEMLAUMU  BW, JAMMEH  KWA  UKIUKWAJI  WA  HAKI  ZA  WATU  WA   MAPENZI  YA  JINSIA  MOJA  ,WAANDISHI  WA  HABARI  NA  WANASIASA WA  UPINZANI.

RAISI  MTEULE  WA  GAMBIA  AMEWAHIMIZA  WATU  WALIOTOROKA  GAMBIA  KWASABABU  YA  HALI  NGUMU  YA  MAISHA YA  MTANGULIZI  WAKE  KURUDI  NYUMBANI  ILI  KUSAIDIA  KUJENGA  TAIFA  LAO  

BWANA  BARROW  ALILIAMBIA  SHIRIKA  LA  HABARI  LA  ASSOCIATED  PRESS  KUWA  ATAWAACHILIA  KUTOKA GEREZANI  WANASIASA  WOTE  WA  UPINZANI  WALIO  GEREZANI

YEYEPIA  ALISISITIZA  KUWA  ATABADILI  MSIMAMO WA  AWALI WA  BW JAMMEH  WA  KUTAKA  KUONDOA  GAMBIA  KATIKA  MAHAKAMA  YA  KIMATAIFA  YA  UHALIFU  WA  KIVITA  ICC  NA  JUMUIYA  YA  MADOLA.

RAIA  WENGI  WA  GAMBIA  WALIKESHA  USIKU  WOTE  WAKISHEREKEA  KUONDOKA  KWA  BW  JAMMEH  AMBAYE  AMESEMA KUWA ATAENDELEA  NA  SHUGHULI  ZAKE  ZA  KILIMO.

LAKINI  CHANGAMOTO  NYINGI  ZIPO


TAIFA   HILO  NI   MASIKINI  SANA  NA  WANANCHI  WENGI   WACHANGA  WAMETOROKEA   MATAIFA  YA   NGAMBO.

No comments:

Post a Comment

Total Pageviews